Thursday, July 28, 2011

RAIS AMUITA IRENE UWOYA IKULU

Rais wa Burundi,Piere Nkurunzinza hivi karibuni alimuita ikulu mwigizaji super star wa filamu kutoka Bongo,IRENE UWOYA(pichani) akimtaka aende ikulu kwa ajili ya mazungumzo nae,Blog hii ina full madata.
Akizungumza na Blog hii julai 27 mwaka huu, Uwoya alisema Rais Nkurunzinza alimuita baada ya kusikia kuwa yupo nchini kwake na kuvuta hisia za wengi.
"Nilipokwenda Burundi kwa ziara ya kisanii,Rais Nkurunzinza alipata taarifa kuwa nimetingisha sana nchini kwake,kutokkana na hilo alitaka kuniona,alinitumia gari na ulinzi wa polisi ili waje kunichukua" Alisema IRENE UWOYA.

MISS:SIWEZI KUWA MALAYA KAMA WEMA

Miss Vodacom kanda ya mashariki,Loveness Flavian (pichani),amesema awezi kuwa na skendo mbovu kama miss Tanzania 2006 Wema Sepetu zinazomwandama kila kukicha na kuonesha sura mbaya ya tasnia ya urembo.
Loveness alisema hivi karibuni kuwa, skendo anazozifanya Wema zinasababisha baadhi ya watu kuchukia mashindano ya urembo kwa imani kuwa kuwahusisha wasichana wasio na maadili mema katika jamii.(picha na moudy likoko)

Wednesday, July 27, 2011

BUNGE lageuka uwanja wa vita

Wabunge wa Chadema na NCCR- Mageuzi wakimfokea Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (kushoto) baada ya mbunge huyo kuwataka wabunge hao warudi bungeni ambapo walitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya Mwenyekiti wa Bunge, Sylvester Mabumba kuamulu askari wa bunge wamkamate Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje na kumtoa nje ya ukumbi, bungeni jana mjini Dodoma.
WENJE ATOLEWA KWA NGUVU, MBUNGE CCM ANUSRIKA KUPIGWA
MBUNGE wa Nyamagana (Chadema), Ezekia Wenje, jana alijikuta akitolewa bungeni na askari (wapambe) wa Bunge waliotii amri ya Mwenyeviti wa Bunge, Sylivester Mabumba, aliyeongoza kikao siku hiyo.Katika tukio ambalo ni la kwanza kutokea tangu kuanza kwa Bunge la Kumi linaloongozwa na Spika Anne Makinda, Mbunge wa Ludewa, Deo Filikunjombe (CCM), alinusurika kupigwa na wabunge wa kambi ya upinzani baada ya kuwakejeli Chadena akisema waache mambo ya kitoto.

Mabumba alitoa amri ya Wenje kutolewa nje baada kukaidi amri ya Mabumba kumtaka akae chini mbunge huyo wa Nyamagana alipokuwa akiomba mwongozo, katikati ya mabishano yaliyokuwa yakiwajumuisha wabunge wengine wakati huo.Wakati Wenje akisisitiza kuomba mwongozo kwa maelezo kwamba jambo analotaka kusema "lina maslahi ya nchi", Mabumba ghafla aliwaita askari (wapambe) wa Bunge na kuwaamuru wamtoe nje kwa kukiuka kanuni za Bunge.

Kabla ya kuwaita askari hao, Mabumba ambaye ni Mbunge wa Dole alikuwa amemwamuru mara tatu Wenje akae chini, lakini hakutii akisema: "Nina jambo la dharura ambalo ni kwa maslahi ya Taifa".

"Sargent Ant Arms, mtoe nje mheshimiwa Wenje," alisema Mabumba na hapo askari watatu waliingia na kumtoa nje Wenje, tukio ambalo liliacha kukiwa hakuna utulivu bungeni.

Pamoja na kusindikizwa na askari wa Bunge, baadhi ya wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi walitoka nje wakimsindikiza Wenje.Walipofika nje ya ukumbi wa Bunge walianza kumlalamika kwamba, Mabumba ameshindwa kuongoza Bunge na kudai kuwa anaonyesha upendeleo wa wazi katika uendeshaji wa vikao vya chombo hicho.

Nje ya Ukumbi wa Bunge
Nje ya Ukumbi wa Bunge ilizuka tafrani nyingine iliyosababisha Mbunge Filikunjombe (CCM), kunusurika kupokea kichapo kutoka kwa wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi baada ya kuingilia mazungumzo yao wakati wanajadili suala la Wenje kutimuliwa ukumbini.

“Tatizo lenu ninyi wabunge wa Chadema mnaishia kuwa wabishi kila wakati, jambo ambalo linawapotezea heshima kwa wananchi,’’ alisema Filikunjombe na kuongeza: “Acheni mambo ya kitoto rudini ndani kuendelea na Bunge. Sio kila siku ninyi Chadema tu, watu wamewachoka.’’

Kauli ya ilikuwa kama kumwaga petroli kwenye moto, kwani kundi la wabunge wa Chadema na NCCR Mageuzi ambao kwa wakati huo wakiongozwa na Moses Machali (Kasulu Mjini NCCR), walimvaa kama nyuki mbunge huyo na kuanza kurushiana maneno makali.

“We mjinga kweli, hapa sio wabunge wa Chadema hata sisi wa NCCR-Mageuzi tupo tunachojadili ni maslahi ya nchi sio ushabiki wa vyama, toka hapa mshamba wewe,’’ alisema Machali.

Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Susan Kiwanga, alimwambia Filikunjombe aache hadithi za kijinga kwani wananchi wa eneo lake wanaporwa chuma, lakini yeye (Filikunjombe) anashindwa kuwatetea badala yake anarukia mambo yasiyomuhusu.“Tuondolee ujinga wako hapa, wananchi wako katika maeneo ya Liganga wanaporwa mali usiku na mchana unashindwa kuwatetea leo unapotuambia tuna akili ya kitoto, hivi unataka Watanzania wafe ili ninyi mshangailie,’’alisema Kiwanga.

Wabunge wengine waliomwandama zaidi Mbunge huyo ni, Machali (NCCR-Mageuzi), Peter Msigwa (Iringa Mjini-Chadema), Mariam Msabaha na Susan Kiwanga wote wa Viti Maalum (Chadema) ambao  walimzingira mbunge huyo na kuanza kumrushia maneno ya kejeli.

Hali ilizidi kuwa mbaya baada ya wabunge wengine wa Chadema, Godbles Lema (Arusha Mjini), Joseph Mbilinyi (Mbeya Mjini) na Vicent Nyerere (Musoma Mjini) walipoingilia ugomvi huo na kutaka Filikunjombe awaombe radhi, lakini alikataa.Kama si busara iliyotumiwa na Mbunge wa Kondoa Kusini, Juma Nkamia (CCM) hali ingekuwa mbaya kwani idadi ya wabunge wa Chadema ilipozidi yalisika maneno kuwa mbunge huyo apigwe, ndipo Nkamia alipofika na kuokoa jahazi akimtaka Filikunjombe aondoke katika eneo hilo.

Maelezo ya Wenje
Wenje aliwaambia waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge kuwa kitu alichokifanya hakikustahili adhabu kama aliyopewa kwa kuwa alikuwa sahihi. '' Pale mimi nilikuwa sahihi kabisa kwani sikutaka kuzungumzia suala la Lissu bali nilikuwa nazungumzia suala la masilahi ya Watanzania wote. Ikumbukwe kuwa kuna samaki walioingizwa bila polisi kujua na sasa wako sokoni wananchi wanakula hiyo ni hatari, sasa mwenyekiti anasema kuwa nitoke hajui kanuni yule,'' alisema Wenje.

Mbunge huyo alisema kitendo cha Mwenyekiti kuamuru atolewe nje kwa amri ni kukiuka kanuni na kwamba hajui kwani aliposema suala la dharula ni pale kunapotokea vita si kweli. '' Kanuni ya 47 (1-3) ndiyo niliyotumia na inaniruhusu kabisa kuomba mwongozo huo, kwani wananchi wanaumia halafu tunaambiwa hadi kuwe na vita, kama si umbumbumbu ni nini basi," alihoji Wenje akiwa ameshika kitabu cha Kanuni za Bunge.Kwa upande wake Mbunge wa Arusha Mjini, Godbles Lema (Chedema) alisema kinachomsumbua Mwenyekiti ni kutokujua kanuni.

Chanzo cha mtafaruku
Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (Chadema) ndiye aliyeanzisha balaa ndani ya ukumbi wa Bunge baada ya kueleza kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Elimu), Kassim Majaliwa amesema uwongo bungeni.

Lissu alisema Majaliwa alipokuwa akijibu swali lake namba 313 kuhusu michango kwa wananchi, amedanganya kuwa wananchi hawalazimishwi kutoa michango hiyo na kusisitiza kuwa ana ushahidi unaothibitisha kwamba michango hiyo ni lazima.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali haitumii nguvu katika kuwatoza wananchi michango hiyo, bali wanashirikishwa katika kuibua, kupanga na kuendesha miradi yao wenyewe,’’ alisema Naibu Waziri Majaliwa.Baada ya majibu hayo, Lissu alisimama na kulieleza Bunge kuwa Naibu Waziri alisema uongo huku akinukuu barua ya Mkuu wa Wilaya ya Singida iliyotolewa Mei 2,2005.

"Naomba kwanza niseme kwamba mimi namheshimu sana Mheshimiwa Naibu Waziri na kwa kweli huwa nakuwa mzito sana kusema Waziri amesema uongo. Lakini katika majibu haya naomba nitoe tamko kwamba, Mheshimiwa Naibu Waziri ameliambia Bunge hili uongo, na naomba nipewe nafasi ya kuthibitisha uongo huo leo leo, tena kwa ushahidi wa maandishi," alisema Lissu na kuongeza:

"Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba sasa niulize swali dogo la nyongeza".Kabla ya kuuliza swali hilo, Mabumba alisema: "Mheshimiwa samahani naomba... Mheshimiwa umekiri katika maelezo yako kwamba Waziri ameshindwa kukuridhisha, maelezo yake hayalingani na swali lako. Kwa hiyo hutakuwa na nafasi ya swali la nyongeza nimtake Mheshimiwa Waziri, No! Nikutake wewe unipe ukweli kuhusu suala hili".

"Tafadhali naomba uliambie Bunge hili ukweli wa suala hili na bahati nzuri umesema hapo ulipo uko tayari kutoa maelezo haya. Tafadhali nafasi ni yako," alihitimisha Mabumba.

Baada ya kupewa fursa hiyo, Lissu alisema Naibu Waziri, Majaliwa si kwamba ameshindwa kumridhisha na kusisitiza kuwa Majaliwa amesema uongo.

"Ndiyo maneno niliyoyatumia, …Naibu Waziri amesema uongo na uthibitisho ni kwamba mimi mwenyewe hapa Bungeni, nina barua ya tarehe 2/5/2005 iliyoandikwa na aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Singida wakati huo, anaitwa Kepteni James Yamungu, ambayo kichwa chake cha habari kinasema; ‘Amri Na.1 ya Mkuu wa Wilaya ya Singida’ na inalazimisha wananchi kulipa michango".

Kabla hajamaliza kusoma barua aliyokuwa ameishika mkononi, Mbunge wa Mbozi Mashariki, Godfrey Zambi (CCM), aliomba mwongozo akisema kipindi hicho hakikuwa cha kutoa uthibitisho bali wabunge walipaswa kuendelea na mjadala wa maswali.Mwenyekiti alikubaliana na utaratibu huo, hivyo kumtaka Lissu awasilishe maelezo husika na kielelezo cha barua baada ya saamoja.

Hali ilibadilika
Hali hiyo ilimkera Mbunge wa Kasulu Mjini (NCCR-Mageuzi), Moses Machali, ambaye aliomba mwongozo wa Mwenyekiti na kutaka muda uongezwe kwa Lissu kabla ya kutoa uthibitisho wake.

“Mheshimiwa Mwenyekiti, muda uliompa Mheshimiwa Lissu kutoa uthibitisho ni mfupi na kwa kuwa Lissu ni mbunge saa tano anatakiwa kuwa ndani ya ukumbi kuendelea na shughuli za Bunge naomba mwongozo wako,’’ alisema Machali.Mwenyekiti wa Bunge hakukubaliana na ombi la Machali na kusema kuwa hawezi kuomba mwongozo juu ya mwongozo hivyo akasema alichokizungumza ndicho kinatakiwa kutekelezwa.

Yalizuka mabishano kwa muda mrefu kati ya Machali na Mabumba ambayo yalimfanya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Uratibu na Bunge, William Lukuvi, kuingilia kati na kuwataka wabunge kutokuchukulia jambo hilo kwa jazba.

“Unajua hapa wabunge hampaswi kuliona jambo hili kuwa ni kubwa kiasi hicho, kwani hata Lissu anaweza kuomba kwa maandishi kuongezewa muda na akaleta kwa wakati wake,’’ alisema Lukuvi.Hata hivyo, kulikuwepo na majibizano na ukali wa maneno kutoka kwa Mwenyekiti ambaye alimwambia Machali: “Unaongea maneno kama tuko klabu cha pombe, unatakiwa kujiheshimu na kuzungumza kwa utaratibu mheshimiwa mbunge’’.

Wakati hayo yakiendelea, Wenje alisimama akiomba mwongozo lakini alimriwa kukaa chini na baada ya kukaidi, Mabumba aliamuru atolewe nje.

Mabumba ajitetea
Akiahirisha kikao cha bunge jana mchana, Mabumba alitumia takriban dakika kumi kujitetea kuhusu hatua yake ya kumtoa nje Wenje kwamba, alifanya hivyo kwa mujibu wa Kanuni za Bunge baada ya mbunge huyo kukaidi amri yake.

"Kwa mujibuwa Kanuni za majadiliano, mtakubaliana na mimi kwamba, Mheshimiwa Wenje alikiuka kanuni hizo maana alikuwa akibishana na kiti na mimi sikuwa nimempa ruhusa ya kuzungumza," alisema Mabumba huku akiwataka wabunge kuzingatia kanuni za Bunge.Alisema kwa mujibu wa kanuni hizo, Wenje alipaswa kutohudhuria kikao kizima cha jana kama adhabu, lakini kwa kuwa alitii amri ya kutoka nje, alimpunguzia adhabu hiyo hivyo anaruhisi kuhudhuria kikao cha jana jioni.

"Kwa mujibu wa Kanuni zetu, Wenje alipaswa kukosa kikao cha siku nzima ya leo (jana), lakini kwa kuwa ametii amri ya kutoka nje na mpunguzia adhabu hiyo anaweza kurejea ukumbini kuhudhuria kikao cha jioni kuanzia saa 11," alisema Mwenyekiti huyo wa Bunge.Hata hivyo, alisema katika mazingira aliyomkatalia Wenje kutoa hoja yake, alikuwa sahihi, kwani haikuwa rahisi kufahamu kwamba hoja ya mbunge huyo ni tofauti na kile kilichokuwa kikiendelea wakati huo.

"Wakati mwingine mazingira huwa ni magumu sana, ni kwa vipi mtu angeweza kufahamu kwamba  alichokuwa akitaka kusema Wenje ni tofauti na hoja ya Mheshimiwa Lissu, ilikuwa vigumu sana," alijitetea Mabumba.

SALA YA WATANZANIA WENGI SIKU HIZI!!!


Eeh Tanesco uliyeko Ubungo,Jina lako ni kuu sana Ufalme wako unaheshimiwa,Mwanza hadi  Sumbawanga. Utakalo lifanyike ila si hili la kutukatia Umeme bila ratiba. Utupe umeme wetu wa kila siku,utusamehe kutukatia umeme 24hrs. Usitutie katika vishavishi ya kuandamana ,kutaka Ngeleja ajiuzuru....

SUGU: NITUMIE PICHA MSHIKAJI

‎...kama kuna mtu yeyote popote alipo duniani ambaye tuliwahi kupiga picha na mimi kati ya mwaka 1990 mpaka 2005,tafadhali nitumie picha hiyo kwenye email yangu deiwaka@hotmail.com...inaweza kutumika kwenye kitabu changu kipya kinachotarajiwa kutoka hivi karibuni...SUGU:MUZIKI NA MAISHA!...karibu sana uwe sehemu ya historia ya maisha yangu mpaka hapa tulipofika...

TOP BAND LIVE SHOW UBUNGO EXTERNAL DAR


RAIS JAKAYA KIKWETE AMTIA MOYO MWANAFUNZI MLEMAVU MTWARA

Rais,Jakaya Kikwete akimsalimia mwanafunzi mlemavu Mohamed Mnatende anayesoma  kidato cha tatu shule ya sekondari ya Mustafa Sabodo iliyoko mjini Mtwara wakati akizindua shule hiyo.

NAIJA NITE PARTY 2011

J'mosi ya tar 30-7-2011 zitagongwa ngoma  mpwaaaaaaaa  na zote kaliza miondoko ya kinaija naija.
                                               Dont miss it people.

UMEME WALIGAWA BARAZA LA MAWAZIRI

Kauli tofauti zinazotolewa na viongozi wa serikali akiwemo Rais Jakaya Kikwete na baadhi ya mawaziri kuhusu suala la mgao wa umeme, zinaonesha kutokuwepo uwajibikaji wa pamoja katika baraza la mawaziri.Uchunguzi uliofanywa  na blog hii kuhusu sakata la tatizo la mgao wa umeme nchini imebaini kwamba kauli za viongozi hao wa serikari hawana sauti ya pamoja hivyo kuongeza utata katika kuleta suluhu juu ya suala hili nyeti.

Tuesday, July 26, 2011

CUF, Chadema moto umewaka kumrithi Rostam Aziz,CCM yasema bado haijajipanga.

Siku chache baada ya Spika wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ANNE MAKINDA kutangaza kuwa kiti cha jimbo la Igunga liko wazi kufuatia kujiuzulu kwa Rostam Aziz .
Vyama vya siasa vimeanza mbio za kuwania jimbo hilo. Rostam alijiuzulu nyazifa zake zote ikiwemo ile ya ubunge wa Igunga 13 julai mwaka huu,kutokana na kile alichosema siasa uchwara ya ndani ya chama chake cha CCM, na wiki iliyopita spika Makinda aliiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),kuieleza kuwa kiti hicho cha ubunge, sasa kipo wazi.

Hapa THT Hapa USHER RAYMOND

Hapa THT wakiwa katika picha ya pamoja na USHER RAYMOND pande za ATALANTA U.S.A
Pale kati USHER akiwa na AMIN wa THT

Tiba ya kikombe cha babu, SERIKALI YASEMA HAITIBU KABISA,waliokunywa wamejisumbua bure

Waziri wa afya  na ustawi wa jamii , DK.Hadji Mponda amepasua jipu na kusema hakuna utafiti wowote wa kisayansi unaothibitisha kuwa dawa za asili zina uwezo wa kutibu ukimwi.
Kauli hiyo ilitolewa na waziri huyo wakati anazindua kituo cha matibabu ya wagonjwa wa ukimwi na mafunzo katika hosipitali ya mnazi mmoja, jijini Dar es salaam mwishoni mwa wiki ilyopita.

TAMASHA LA EPIQ NATION LAZUA GUMZO SINZA


                                            CP akitema swagga jukwaani
Tamasha le epiq Nation linalotayalishwa na mtandao wa kampuni ya simu za mikononi, Zantel, lililofanyika juzi katika viwanja vya TP Sinza Darajani,Jijini Dar es salaam, ambako lilivutia wapenzi wengi sana wa burudani.

KILO 1000 ZA SAMAKI WENYE SUMU WASAMBAZWA NCHINI

                                             Katibu mkuu wizara ya afya na ustawi wa jamii Blandina Nyoni.
Wizara ya afya na ustawi wa jamii imetahadharisha kusambazwa kwa samaki wenye sumu sehemu mbalimbali  nchini na kuwataka wananchi washiriki msako ulioanzisha kuwatafuta.
Taarifa ya wizara hiyo iliyotolewa jana jijini Dar es salaam ,imeeleza kuwa samaki hao ni sehemu ya kilo 124,992 zilizo ingizwa nchini kutoka Japan.

Friday, July 22, 2011

WANACHUO HILI NI BONGE LA SUPPLIES KWENU

BANANA ZORO AWATEMA

Msanii maarufu bongo Banana zoro amefuta mpango wake wa kuwarudisha waimbaji wa zamani wa bendi yake (BANANA BAND), coz zile zilikuwa akili za kibabu.

AUNT EZEKIEL SASA NI UROJO MPAKA KIELEWEKE

Msanii maarufu wa filamu Bongo, Aunt ezekiel sasa adaiwa kula urojo kufuatia kutokukaukiwa na skendo zinazowahusisha wanaume kila kukicha.
Hilo limebainika kufuatia na kitendo kilichotokea hivi karibuni  cha mwanadafada huyo na msanii mwenzake, Yusuph Mlela kunaswa 'live' wakifanya mambo ya mahaba mbele ya kadamnasi .
Laana hiyo ilitokea ndani ya viwanja vya leaders club, kinondoni  jijini Dar es salaam ambapo wasanii hao waligandana kama ruba  muda mchache wakaonekana katika mazingira ya utata yaliyo ach vingi viulizo kwa watu waliokuwa wanapiga chabo.by likoko inc.

SHILOLE "AMTAPIKA"BARNABA

Msanii wa filamu kitaa cha BONGO,Zuwena Mohamed "shilole" pichana amemtapika aliyekuwa mpenzi wake Elias Barnaba kwa madai kuwa hivi karibuni amemdhalilisha.
Akigonga story na mdaku wetu jana shilole alisema kuwa ,uhusiano wa kimapenzi kati yake na Barnaba haukuwa na kificho ila kwa kuwa ameonesha kutokuwa na msimamo  anaona bora waachane tuu.
Aliendelea kudai kuwa Barnaba ni mwanaume aliyezaliwa na tamaa na yeye ndiye aliyemchoka kwa hivyo anamsubiri akirudi kutoka marekani, wanaachana rasmi.

CHUJI AWEKWA CHINI YA ULINZI VILLA SQUARD

Baada ya villa squard kumnasa kiungo Athuman Idd "chuji", (pichani) kocha mkuu wa timu hiyo, Juma Pondamali ametamba yeye ndio kiboko ya wachezaji  wa  aina ya kiungo, hivyo na kudai atafanya jitihada za kutosha anambadili tabia.
Pondamali ambaye ni kocha wa makipa wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa stars, amesema simba na yanga zimeshindwa kumbadilisha chuji anayedaiwa kuwa ni  mkorofi ,hivyo amezitaka kusubiri kuona mabadiliko ya muda mfupi kweye ligi kuu.

Thursday, July 21, 2011

PINDA: Hatima ya Divid jailo iko kwa raisi.

Waziri mkuu Mizengo Pinda anayaweke hadharani maagizo aliyopewa na Raisi jakaya kikwete kuhusu tuhuma za rushwa zinazomkabili katibu mkuu wa wizara ya nishati na madini David jailo, Pinda  ameambiwa  hatulie swala hilo hatalishughulikia raisi mwenyewe  atakapotoka ziarani afrika kusini.tuhuma za jailo ziliibuliwa nambunge wa kilindi (ccm) Beatrice shelukindo ambaye alisema jailo ameziandikia barua idara na taasisi hizo akiagiza ziweke fedha hizo kwenye akaunti namba 5051000068 inayomilikiwa na Geological survey of tanzania (GST) kwenye benki ya NMB, tawi la Ddoma.  habari zaidi na Moudy Likoko.
yaani ni mwanzo mwisho full kuuza

FULL MAUZO NA BONGO255

wooow king a.k.a mfalme wa la familia kutoka kitaa cha ilala akiwa katika makamuzi ya serengeti fiesta dat wats up

Wednesday, July 20, 2011

yeees godizila  a.k.a  kingzila na makamuzi ya serengeti fiesta pande za mwanza mwanza

bongo255

Maisha ni safari ndefu na katika maisha mtu unatakiwa kumuomba mungu sana ili akusaidie na mungu mkubwa humpa kila haombaye kwahiyo najua one mungu hatanijalia kufikisha ndoto zangu mungu mkubwa    in god i trust    amin.