Tuesday, July 26, 2011

CUF, Chadema moto umewaka kumrithi Rostam Aziz,CCM yasema bado haijajipanga.

Siku chache baada ya Spika wa Bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania, ANNE MAKINDA kutangaza kuwa kiti cha jimbo la Igunga liko wazi kufuatia kujiuzulu kwa Rostam Aziz .
Vyama vya siasa vimeanza mbio za kuwania jimbo hilo. Rostam alijiuzulu nyazifa zake zote ikiwemo ile ya ubunge wa Igunga 13 julai mwaka huu,kutokana na kile alichosema siasa uchwara ya ndani ya chama chake cha CCM, na wiki iliyopita spika Makinda aliiandikia barua Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC),kuieleza kuwa kiti hicho cha ubunge, sasa kipo wazi.

No comments:

Post a Comment